IQNA

Mashindano ya Kitaifa ya Qur'ani  Brunei yahimiza Waislamu kupenda Qur’ani

17:14 - February 14, 2025
Habari ID: 3480217
IQNA – Mashindano ya kitaifa la kuhifadhi Qur'ani nchini Brunei yana lengo la kujenga upendo wa kina kwa Qur'ani miongoni mwa Waislamu, hasa wanafunzi, vijana, wataalamu na watumishi wa umma, afisa mmoja alisema.

Hili linahimizwa kwa kuwahamasisha kuhifadhi na kuelewa mafundisho yake, alisema Mkurugenzi Mshiriki wa Kituo cha MABIMS cha Masomo na Usambazaji wa Qur'ani Mohammad Ali Sabri Yusof Jumatano.

Akitoa hotuba yake katika hafla ya kutoa zawadi za shukrani kwa washiriki na vyeti kwa majaji wa mashindano ya  mwaka huu, alisisitiza kwamba mashindano hayo yanaendana na maono ya Sultan Hassanal Bolkiah Mu'izzaddin Waddaulah ya kuongeza idadi ya wahifadhi Qur'ani nchini Brunei.

Hafla ilianza kwa kisomo cha Surah Al-Fatihah na Imam Manan Osman kutoka Msikiti wa Sultan Sharif Ali, Sengkurong, ikifuatiwa na shindano la Kategoria ‘E’, ambapo washiriki watano – wanaume watatu na wanawake wawili walishindana.

Mashindano ya mwaka huu yalikuwa na washiriki 25 katika kategoria tano, ikijumuisha washindani 16 wa kike, ikionyesha ushiriki mkubwa kutoka kwa wanawake katika kuhifadhi Qur'ani.

Hafla iliyofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (ICC), Berakas, iliashiria hitimisho la shindano la siku mbili, lililoanza Februari 11.

Naibu Waziri wa Masuala ya Kidini Pengiran Datuk Seri Paduka Mohd Tashim Hassan, mgeni rasmi, alitoa tuzo kwa washiriki na majaji.

Maafisa wakuu kutoka Wizara ya Masuala ya Kidini (MoRA), wawakilishi kutoka mashirika ya serikali na taasisi za elimu pia walihudhuria.

Mashindano hayo ya kila mwaka yaliandaliwa na MoRA kupitia Kituo cha MABIMS cha Masomo na Usambazaji wa Qur'ani,  na ni mpango muhimu unaoelekea kwenye Sherehe ya Kitaifa ya Nuzul Al-Qur'ani katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Lengo ni kuhimiza usomaji wa kila siku wa Qur'ani, kukuza ufahamu wa maana yake, na kueneza utamaduni wa kuhifadhi miongoni mwa watoto, vijana, na jamii kwa ujumla kupitia mashindano salama.

3491853

Kishikizo: brunei qurani tukufu
captcha